Soka kama mchezo wowote mwingine vinahitaji kipaji na kufanya kwa bidii lakini juu ya hayo yote ni nidhamu kwanza. Uvutaji sigara haukubaliwi katika amali hii lakini baadhi ya watu wachache wanaendelea kuvunja sheria na kushiriki katika tabia hii nyuma ya pazia. Wachache walikamatwa lakini wengi wanaendelea. Hapa chini kuna orodha yetu ya wachezaji wavutaji sigara kuliko wengine.

1. Mario Ballotelli

Balo-Smokes

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli alipigwa picha mara nyingi akivuta sigara na si jambo la kushangaza kuwa anashikilia nafasi ya kwanza katika orodha hii.

Kwa sasa anacheza kwa vigogo wa SERIE A AC Milan ambapo hucheza kama mkopo kutoka Liverpool ya Ligi Kuu ya England.

2. Jack Wilshere

Wilshere-Smokes

Mwenye umri wa miaka 24 kiungo wa Arsenal Jack Wilshere alipatikana katika habari na magazeti mara nyingi kwa sababu mbaya katika miaka ya hivi karibuni. Kama si jeraha kali, yaweza kuwa shida ya nidhamu. Uvutaji sigara, Shisha au hata kuwatukana mashabiki wa Tottenham Hotspur, Wilshere huonekana kama ni mtu wa kuvutia habari mbaya zote. Ni mchezaji mwenye kipaji na angekuwa na mustakabali mzuri lakini tabia zake hazimruhusu kamwe. Alishauriwa na wachezaji wastaafu hata na mameneja mara nyingi lakini inaonekana kwamba maonyo yote yanaangukia masikioni mwa kiziwi.

3. Mesut Ozil

Ozil-Smoker

Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil pia yuko katika orodha ya wachezaji wavutaji sigara. Ni aina ya mchezaji anayeonekana kama anaweza kuficha kila kitu lakini hawezi ficha mapenzi kati yake na sigara. Hii yaweza kuwa sababu inayomfanya kila wakati aonekane kama kama mwenye shida ya kupumua.

4. Wojciech Szczęsny

Scezny

Arsenal ina mchezaji mwingine katika orodha. Huu ni wakati wa Golikipa Wojciech Szczęsny ambaye kwa sasa hucheza kwa AS Roma kama mkopo. Mara nyingi alishauliwa na meneja Wenger aliyekuwa mvutaji pia lakini anashindwa kuachilia tabia hiyo.

5. Fabio Coentrao

Coentao-Smokeee

Beki wa Real Madrid Fabio Coentrao naye hupatikana katika orodha hii. Kwa sasa hucheza katika AS Monaco kutoka Ligue 1. Ni mchezaji wa kudumu katika timu ya taifa ya Ureno.

6. Lionel Messi

Messi-Smoke....

Hakuna taarifa nyingi zaidi kuhusu maisha ya uvutaji wa nyota wa Barcelona lakini ukweli ni kwamba anavuta sigara na mapaparazi walimnasa mara nyingi kwa kamera akivuta.

7. Wayne Rooney

Rooney-Smoke

Nahodha wa England na Manchester United Wayne Rooney hupatikana kila mara katika matukio asiyo ya kawaida. Isipokuwa michezo ya kupigana ngumi, zinakuwa kadi nyekundu za ujinga, ulaghai dhidi ya mke wake au kudumu miezi kadhaa bila kufunga mabao.

Alianza tabia za uvutaji sigara angali kijana chipukizi na kwa mujibu wa habari zitokazo karibu naye, Rooney alikuwa na shida kubwa na meneja wa zamani Sir Alex Ferguson. Ripoti zinazoaminika zinaonyesha kuwa aliacha tabia hiyo lakini wengine wanasema kuwa bado anavura sigara kisiri.