Kwa kawaida tunazoea kwamba wachezaji wa soka hawasomi kufika kiwango cha juu isipokuwa kumaliza shule za msingi au za sekondari. Lakini kuna wachache wanaoweza kufikia kiwango cha juu katika elimu. Hapa kuna orodha ya wachezaji 10 wanaokuwa na elimu ya juu kuliko wengine.

10.Nedum Onuoha

Nedum

Beki wa QPR Nedum Onuoha alishinda masomo kumi kwa kiwango cha juu katika ratiba ya shule za upili(GCSE), kukiwemo nane aliyoshinda kwa kiwango cha A na mawili kwa kiwango cha B.

Kwa kiwango cha A alipata A katika masomo matatu, katika Hisabati, Stadi za Biashara na teknolojia. Alama zake zinamruhusu kuhudhuria takribani chuo kikuu chochote nchini Uingereza.

He has qualification to attend almost any university in England.

9.Simon Mignolet – Shahada katika Sheria

Simon Mignolet

Golikipa wa Liverpool Shahada katika Sheria na  Sayansi ya Kisiasa, na anaweza kuzungumza lugha nne: Kiingereza, Kifaransa, Kiholanzi na Kijerumani.

8.Shaka Hislop – Shahada ya Heshima  katika Uinjinia Magari

Trinidad and Tobago's goalkeeper Shaka H

Golikipa wa zamani wa Newcastle United ana Shahada katika Uinjinia wa Magari kutoka Howard University. Kwa sasa, hutumika kama mchambuzi wa mambo ya soka kwenye ESPN.

7.Iain Dowie – Shahada ya Uzamili katika Uhandisi

Iain Dowie

Mshambuliaji wa zamani wa Southampton, West Ham na QPR humiliki Shahada ya Uzamili katika Uhandisi kutoka Southampton University.  Alijulikana pia kama mtu aliyetumika katika Kampuni ya Huduma za Anga nchini Uingereza(British Aerospace).

6.Steve Coppell – Shahada katika Mambo ya Uchumi

Bristol City v Blackpool - Pre-season Friendly

Coppell alicheza katika Manchester United mnamo mwisho wa 1970 na mwanzo wa 1980. Humiliki Shahada katika Mambo ya Uchumikutoka University of Liverpool.